Twaja kwako Bwana (leo) kwa furaha kubwa (sisi)
Twaleta zawadi Bwana tukushukuru
Kwa Baraka zako (zote) nayo mema yako (kwetu)
Kweli u mkarimu Bwana masihani mwetu.
Twajitoa kwako, Bwana utupokee sisi
Japo hatustahili, twaja ututakase
Nafsi zetu sisi, twazitoa kwako ee Bwana
Ili iwe ishara, ya shukrani zetu kwako
Mkate mazao ya ngano, tunakutolea Bwana
Upate kugeuza uwe mwili wako Bwana.
Kutoka kwa mizabibu tunaleta na divai, Bwana uigeuze
Iwe kinywaji cha roho, tupate uzima wako
Kutoka kwa mifuko yetu, tunakutolea fedha
Kama fungu la kumi, Bwana zibariki zote
Kutokana na bidii zetu tunakutolea mazao ya mashamba
Kutoka kwa boma zetu, twaleta mifugo kwako
Tunajitoa kwako Bwana kwa nafsi na maisha yetu,
Pia na nguvu zetu tuwe watumishi wako
Mioyo yetu twaleta kwako tupokee Bwana, sisi ni waja wako
Tutumie jinsi wewe utakavyopenda Bwana.n
Zawadi tuletazo kwako kwa moyo wa ukarimu
Tunakuomba Bwana nazo zipokee kwako
Utujalie Baraka pia na fadhili zako, wewe ni Mungu wetu
Nasi tutaishi daima ndani yako Baba yetu