SectionsExitTuvumiliane

Tuvumiliane

Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Easter,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Christmas,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Easter,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,MarianExit
Chorus

Tuvumiliane tuvumiliane, tuishi kwa upendo nao wenzetu

Tuwakubali hao jinsi walivyo, ijapokuwa hawafanani nasin

Verse 2

Wapo walio masikini wahitaji, miongoni mwetu

Tusiwachoke wanapoombaomba, tuwavumilie

Wengine hawana elimu kama sisi, miongoni mwetu

Tuwaeleze kwa upole na pia, tuwavumilie hivyo

Verse 3

Wengine wa asili tofauti nasi, miongoni mwetu

Tusizidharau tamaduni zao, tuwavumilie

Pia wapo wengi wa dini mbali mbali, miongoni mwetu

Tusiwahukumu kwa imani yao, tuwavumilie hivyon

Verse 4

Malezi na mapito yetu sio sawa, miongoni mwetu

Wengine wameona machungu mengi, tuwavumilie

Wengine hukasirika haraka sana, miongoni mwetu

Tusiwe sababu ya machozi yao, tuwavumilie hivyo