Tutawapeni Pesa
Haya enyi makamanda, leteni mchango wenu *2
Nguvu ya hoja itawa-ale,
Hawa walinzi wameleta habari kuwa kweli amefufuka, amefufuka *2
Sikieni mimi natoa hoja ya nguvu, hoja yangu kweli ya nguvu
Jambo hili likisikika, likisikika katika Uyahudi
Na Samaria itakuwaje aibu hiyo elezeni *2
Hivyo ninyi walinzi, seme-ni
Wanafunzi wake wamemwiba Bwana wao *2
Sisi tulipokuwa tumelala *2
{ (Tutawapeni mapesa) tutawapeni mapesa,
Tutawajaza mapesa, mapesa mtajazwa } *2
Na msiogope kwa ajili ya hilo * 2n{ Wakuu wa nchi wakisikia tutaongea nao
Wakuu wa nchi hao tutasema nao } *2na. Siku ile ya kufufuka Bwana, maaskari walitetemeka
Wakaenda kwa upesi kumwona jemedari mkuu kumpasha habari
b. Jemedari akafadhaika akawaita watu pamoja kwa shauri;
Wakafanya shauri juu ya jambo hili lipate sura, sura mpya.
c. Dunia yetu siku hizi yafananaje na haya mambo yaliyotokea;
Ukweli unapindishwa ili lile la uongo liwe kwelin