SectionsExitTutaipataje Amani

Tutaipataje Amani

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Chorus

Waumini na mataifa yote na jumuiya zo-te

Kama chemi chemi mo-ja, na tutafakarini pamoja } *2n

Tutaipataje amani kwa bunduki nayo mabomu

Tutaipataje amani kwa migogoro ya siasa

Oooh inasikitisha, tumuombe Mungu atupe hekima

Oooh enyi mataifa, tumuombe Mungu atupe amani

Verse 2

Mapanga hata marungu hayatasaidia, kupata amani

Ugomvi kwa majirani hautasaidia, kupata amani

Tuweke silaha chini tumuombe Mwenyezi, atupe hekima

Tukae chini na wenzetu tujadiliane, tupate amani ae

Verse 3

Makabila kupigana haitasaidia, kupata amani

Mataifa kupigana haitasaidia, kupata amani

Mzungu na Mwafrika sisi sote ni ndugu, tuombee amani

Afrika na Ulaya sisi wana wa Mungu, tuombee amani ae

Verse 4

Jumuiya mbalimbali tuungane pamoja, tuombee amani

Afrika Mashariki nayo isiwe nyuma, tuombee amani

Tanzania nayo Kenya sisi wana wa Mungu, tupendane sote

Dunia yote sisi sote ni wana wa Mungu, tupendane sote ae