SectionsExitTusonge Mbele

Tusonge Mbele

Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,MarianExit
Verse 1

Ingawaje ni mbali sana, mbinguni penye makao mazuri

Lakini tunapatamani, tutafika na tutaishi milele

Ina milima na mabonde, njia inayoelekea huko

Lakini tunajitahidi, hatusitishwi, hatukati tamaa aya aya heen

Chorus

n{

Tunakanyaga, tunasonga hatulali

Tunakwenda, tunasonga hatulali

Polepole, tunasonga hatulali

Taratibu, tunasonga hatulali }* 2

Verse 3

Kanuni tumezisikia, na tunajitahidi kuzishika,

Tukiteleza twainuka, hatulali na hatufungi ukope

Kuwapenda jirani zetu kupoteza kusudi wafaidi

Kama Yesu alivyofanya, akakuja na kufa msalabani aya aya heen

Verse 4

Hatutakwi kuzubaa, dunia siyo makao yetu

Tumeletwa kutumikia, kuondoka na kurudi kwake Mungu

Iwe isiwe tutafika, kwa sababu njiani ni kweupe

Kulisafishwa Kalvari, hakika tu ni kupita bila shaka aya aya hee