Tunakutukuza

Ordinary Time,MarianThanksgiving
Verse 1

Pande zote za dunia, viumbe wako wote wakushangilia,

Watu wanakuinua, nasi tunakuimbia;

Umekuwa mwaminifu, watukumbuka sisi tulio dhaifu,

Tusojua kukusifu, wewe mwenye utukufu.n

Chorus

Kwa zeze na vinanda - tunakutukuza

Baragumu na panda - tunakutukuza

Nderemo zimetanda - tunakutukuza

Na ngoma zinadunda - tunakutukuzan

Iyee (ae hoye) , aiyee (ae hoye ) aiyee (ae hoye) tunakutukuza

Aiyee (ae hoye) , aiyee (ae hoye ) aiyee (ae hoye) tunakutukuza

Verse 3

Sina budi kushukuru, ulinivua giza kanivika nuru,

Utumwa kaninusuru, kaniweka niwe huru;

Japo mimi hukosea, hujanitupa bado wanihurumia,

Hata ninapopotea, wanielekeza njia.n

Kwa nyimbo na zaburi - tunakutukuza

Filimbi na zumari - tunakutukuza

Kayamba na matari - tunakutukuza

Verse 4

Unipaye bure hewa, kunitetea kila ninapoonewa,

Kwako sijapungukiwa, wala sijaelemewa;

Unayenipa mkate, na kunilinda kote wakati wowote,

Nijalie nisisite, kukusifu siku zote.n

Sifa zote ni zako - tunakutukuza

Huko juu uliko - tunakutukuza

Vigelegele, heko - tunakutukuza

Na shangwe na chereko - tunakutukuza

Chorus

n* * *

Verse 6

Una neema tele - tunakutukuza

Tangu enzi za kale - tunakutukuza

Na umebaki vile - tunakutukuza

Milele na milele - tunakutukuza

Verse 7

Wasio na chakula - unawapokea

Wasona pa kulala - unawapokea

Wajapo kwako bila - unawapokea

Unawajibu sala - unawapokea

Chorus

* * *

Verse 9

Vipofu wanaona - wanakutukuza

Viwete wanapona - wanakutukuza

Tasa wapata mwana - wanakutukuza

Na bubu wananena - wanakutukuza

Verse 10

Kweli wewe ni baba - tunakutukuza

Daima watubeba - tunakutukuza

Kwako twapata tiba - tunakutukuza

Watukinga misiba - tunakutukuza