Verse 1
Tunakuja na vipaji vyetu, mbele zako ee Bwana
Tunatoa shukurani zetu, kwako Baba Muumba
Chorus
Tunaleta mavuno, Bwana Mungu pokea
Tunaleta na fedha, Bwana Mungu pokea
Mkate na divai, Twakuomba upokee
Verse 3
Ni matunda ya mashamba yetu, uliyotujalia
Ndilo jasho letu sisi Bwana, twakuomba pokea
Verse 4
Watumishi wako tunakuja, na zawadi kidogo
Twakusihi sana Mungu Baba, pokea mikononi
Verse 5
Nafsi zetu zote mali yako, utupokee sisi
Ee Bwana utujalie afya, uzima na barakan