Tunaishi Kwa Amani
(Tunaishi pamoja kwa amani ee ndugu yangu,
Kama jumuiya moja, kwa pendo la Mungu *2)
Ona, {Tumeunganishwa (sote)
Kwa pendo lake Muumba, Sasa,nkwa nini tufarakane
Kwa mambo yatutengayo na Mungu }*2
Ugomvi kati yetu unatoka wapi,
Mbona sisi sote ni watoto wa Baba mmoja
Kwa nini tugombee mali za dunia
Tukumbuke pendo lake Mungu, tuondoe tofauti zetu
We baba nawe mama mwagombea nini
Mbona mwasahau ahadi yenu siku ya ndoa
Ugomvi wenu unaathiri watoto
Kumbukeni pendo lake Mungu, muondoe tofauti zenu
Makasisi, watawa mwatafuta nini
Mbona mwasahau ahadi nazo nadhiri zenu
Ubinadamu mbona unawatawala
Kumbukeni pendo lake Mungu, m'mkabidhi maisha yenu,
Ugomvi wa kidini unatoka wapi
Mbona sisi sote ni raiya wa taifa moja,
Kubagua kabila, rangi ni kwa nini
Tukumbuke pendo lake Mungu, tuondoe tofauti zetu
Sasa enyi vijana mwatafuta nini
Mbona matendo yenu mengi ni chukizo kwa Mungu,
Hamuheshimu wazazi na Mungu wenu
Kumbukeni pendo lake Mungu, m'mrudieni Mungu wenu