Verse 1
Tumwangalie Mkombozi akitundikwa msalabani
Tutatambua upenzi aliotupenda moyoni.
Chorus
{ Twimbe, twimbe jamani
Salaam, Yesu, msalabani } *2
Verse 3
Msalaba sio mtiwe, tunaotaka kuheshimu,
Ila ni Yesu mwenyewe, kwa binadamu amwaga damu.n
Verse 4
Tuusifu sana mti huu, Yesu akauchagulia
Kwa mapendo yake makuu, deni zetu kuzilipia.
Verse 5
Kwa stahilize msalaba, twapata msamaha wa dhambi
Ni Yesu mwenye kumwomba Babaye Mungu wetu Rabbi.