{ Ni nani mwanadamu mwenye nguvu kuliko Mungu (hakuna) } *2
Ajitokeze mbele za watu tumuone, hakuna
Iyelele iyele, iyelele iyele - hakuna *4
Ni Mungu tu awezaye yote hivyo tumwogope
Huu ndio ukweli kwa wanadamu wote
Analopanga Mungu mwanadamu halipangui
Akipanga uwe padri, utakuwa wewe padri
Akipanga we mtawa, utakuwa we mtawa, muogope Mungu
Huu ndio ukweli kwa wanadamu wote
Analopanga Mungu mwanadamu halipangui
Akipanga uwe raisi, utakuwa we rais
Akipanga uwe waziri, basi wewe ni waziri, muogope Mungu
Huu ndio ukweli kwa wanadamu wote
Analopanga Mungu mwanadamu halipangui
Akipanga uwe mbunge, basi wewe ni mbunge
Akipanga uwe balozi, utakuwa we balozi, muogope Mungu
Huu ndio ukweli kwa wanadamu wote
Analopanga Mungu mwanadamu halipangui
Akipanga uwe tajiri, basi wewe ni tajiri
Akipanga uwe maskini, utakuwa maskini, muogope Mungu
Huu ndio ukweli kwa wanadamu wote
Analopanga Mungu mwanadamu halipangui
Akipanga kukurudisha, mavumbini utarudi
Analopanga Mwenyezi, daima halipingiki, muogope Mungun