SectionsThanksgivingTumshukuru Mungu (Ii)

Tumshukuru Mungu (Ii)

Ordinary Time,MarianThanksgiving
Verse 1

Tumshukuru Mungu kwa ukarimu wa-ke (pia)

Pia na wema wake kutupenda namna hii

Chorus

{ Nitazame - nitazame mimi (kisha ) nawe jitazame } *2n(waweza) kuwa umeo-na (kama) tuko tofauti sura

Nna hata matendo ( yetu) ni tofauti kweli

Lakini Mungu wetu - wala habagui

Anatupenda sote - ni vyema kumshukuru

Verse 3

Matendo yake hayachunguziki, Mungu wetu (kweli)

Kweli hatupaswi kuyachunguza mambo haya

Verse 4

Mawazo yetu sisi yana upeo wake (wala)

Hatuwezi kujua siri za Mungu wetu

Verse 5

Twapaswa kushukuru kwa vyote tulivyo navyo

Kwani kila kitu tumepewa na Mungu pekee