SectionsExitTumshangilie Maria

Tumshangilie Maria

Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Christmas,Christmas,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Lent,Baptism,Christmas,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary TimeExit
Verse 1

Ni Maria mtakatifu, tumshangilie Maria

Ni mzazi wa Mungu Mwana

Ni mkuu wa mabikira

Ni mama yake Yesu Kristu

Chorus

Vigelegele vifijo na makofi

Hoye hoye nderemo nyingi

Pia vifijo tumshangilie Mama Maria

Yeye ni mwombezi wetu na msaada

Njooni tumwimbie chereko maman

Verse 3

Mama wa neema ya Mungu -

Mama mtakatifu sana -

Mama wa usafi wa moyo -

Mama usiye na doa -n

Verse 4

Ni mama usiye na dhambi

Pia mama mpendelevu

Ni mama msaada wetu

Ni mama wa shauri jema

Verse 5

Ni Mama wa Muumba wetu

Pia mama wa Mkombozi

Bikira wa utaratibu

Ni bikira mwenye heshima

Verse 6

Ndiye bikira mwenye sifa

Ndiye bikira mwenye enzi

Ni bikira mwenye huruma

Na ndiye bikira amini

Verse 7

Na ndiye kioo cha haki

Ni kikao chenye heshima

Sababu ya furaha yetu

Ndiye chombo chenye rehema

Verse 8

Ndiye chombo chenye heshima

Ni chombo chema cha ibada

Ndiye waridi lenye fumbo

Ndiye manara wa Daudi

Verse 9

Yeye ni mnara wa pembenyeye ni nyumba ya dhahabu

Ndiye sanduku la agano

Yeye ni mlango wa mbingu

Verse 10

Ndiye nyota ya asubuhi

Yeye ni afya ya wagonjwa

Kimbilio la wakosefu

Mfariji wa wenye uchungu

Verse 11

Ni msaada wa Wakristu

Malkia wa malaika

Ndiye malkia wa mababunmalkia wa manabii

Verse 12

Ndiye malkia wa mitume

Malkia wa mashahidi

Malkia wa waungama

Malkia wa mabikira

Verse 13

Malkia wa watakatifu

Aliyepalizwa mbinguni

Ni wa Rosari takatifu

Ndiye Malkia wa amani