Chorus
Tumkimbie (tumkimbie) huyo huyo shetani (kimbia)
Shetani ameleta mafarakano katika dunia hii *2
Chuki zimetawala ee Bwana, magonjwa ni mengi sana
Tufanye nini tuepuke na matatizo haya *2
Verse 2
Tumeyasahau maagizo ya Bwana wetu Yesu Kristu
Aliyotufundisha sisi wanadamu, Ndiyo maana kuna machafuko
Verse 3
Mwenye masikio na ayasikilize maneno ya Bwana
Mkatende kama alivyotenda yeye, Dunia itakuwa na amani
Verse 4
Tungeishi na amani kama samaki katika bahari
Dunia hii ingekuwa ni paradise, Kama bustani ile ya Edeni
Verse 5
Tumelia sana Bwana hata machozi hayatoki tena
Tufanye nini sisi ni viumbe wako, Njoo haraka utusaidie