Tumesisimka

BaptismOffertory
Chorus

{ Tumesisimka (kweli) tunakuja kwako ee Baba

Tumeandama (sote) tunaleta zawadi zetu

Waumini wote simameni twende pamoja,

Tupeleke fedha mavuno na mifugo yetu } *2

Verse 2

Ondokeni Baba na mama ondokeni nanyi watoto

Chukueni fedha na mali, tupeleke mbele za Bwana

Tuweke akiba mbinguni, nasi tutabarikiwa *2

Verse 3

Hima hima twende pamoja, hima hima twende kwa Bwana

Tupeleke furaha zetu, tupeleke uchungu wetu

Simameni twende kwa Bwana tupeleke nyoyo zetun

Verse 4

Fedha za mifukoni mwetu tupeleke kwa ukarimu

Na mapato ya nguvu zetu, tupeleke kama zawadi

Twende kwake tumshukuru, sote tupate Baraka*2

Verse 5

Mavuno tuliyojaliwa, kutokana na jasho letu

Mifugo tunaowafuga, tupeleke kama sadaka

Tutabarikiwa zaidi, Bwana atatubariki *2n

Verse 6

Mkate mazao ya ngano, divai tunda la zabibu,

Kageuza mwili na damu, tutakula na kubakisha,

Tutapata nguvu zaidi, na uzima wa milele *2