Verse 1
Hawataaibika, wala hawatafedheheka
Milele na milele (milele) wao watashinda magumu
Radi haitawapiga, mvua haitawagharikisha
Milele na milele (milele) wao watashinda mauti
Chorus
Tazama
Hawa ndio wale waliotambua (kuwa)
Bwana Yesu ndiye fimbo ya ushindi (tena)
Na wakakubali kumtumainia (yeye)
Yesu ni mwamba na yeye mshindi (ni)
Yesu kamanda wa wote tumwende yeye
Verse 3
Wamtumainiao, wamechagua fungu jema
Kwani hawatakwama wala kushindwa na lolote
Verse 4
Yesu aliahidi, kutoa kila aombwapo
Naye ni mwaminifu, anayetimiza ahadin
Verse 5
Kuugua kufiwa, si tatizo kwa watu hawa
Ufukara si hoja, kwa wamtumainiao Yesu
Verse 6
Vita wameshavishinda, mapambano wamemaliza
Na wamevikwa taji, wamevikwa taji la haki