SectionsExitTukuzeni Jina Lake

Tukuzeni Jina Lake

Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Chorus

Tukuzeni Jina lake, milele na milele *2

Hubirini kwa watu ajabu zake zote

Semeni Bwana Mungu ni Bwana wa mabwanan{ Tangazeni kwa kuimba, kwa zaburi hata vinanda,

Na tarumbeta pia vinubi vyenye sauti ya kupendeza

Semeni ya kuwa ni Mfalme wa wafalme } *2

Verse 2

Mpeni Bwana utukufu,

Na nguvu pia mpeni, mwabuduni kwa uzuri wake,

Kwa uzuri wa utakatifu, tetemekeeni mbele zake

Verse 3

Mwimbieni Bwana wimbo mpya,

Mwimbieni Bwana wimbo mpya kwa maana ametenda

Ametenda mambo ya ajabu machoni pa mataifa

Verse 4

Paazeni sauti zenu,

Mkiimba kwa furaha, kwa madaha ukirukaruka

Ukicheza na kusimulia matendo yake ya ajabu