Tuidhihirishe Imani
Waamini tunaalikwa, kuidhihirisha imani yetu kwa matendon{Ni mwaliko wa Baba Mtakatifu, ni mwaliko wa Kanisa
Kuipa uhai imani tunayoikiri,nimani tunayoiadhimisha, imani tunayoiishi } * 2
Imani tunayoikiri,
Ndiyo kusadiki kwa Mungu mmoja mwumba Mbingu na nchi
Ndiyo kusadiki kwa Bwana mmoja Yesu Kristu
Ndiyo kusadiki kwa Roho Mtakatifu
Imani tunayoikiri,
Ndiyo kusadiki kwa kanisa moja takatifu Katoliki la mitume
Kuungama ubatizo mmoja, ufufuko wa wafu na uzima wa milele
Imani tunayoadhimisha, ndiyo sakramenti za kanisa
Zilizo chemichemi za neema tupatazo kwa Mungu
Sisi tunaomwamini Kristu na kumfuata
Imani tunayoiishi, ndiyo kuziweka maishani mwetu amri zote za Mungu
Bila kuyumbishwa na hisia za uhuru wa kidunia
Na kubaki katika mtazamo wa Kimungu kwa mafundisho ya kanisa