{ Siku zinapita, miaka yapita
Neno lake Bwana halitapita kamwe }*2
Tu mavumbi sisi, tutarudi mavumbini *2
mmmm mmmm mmm siku hiyo ni ya huzuni mnonmmmm mmmm mmm siku hiyo kweli inatisha
Kwa maana siku hiyo,
Mavazi yako yatakuwa ni sanda
Kitanda chako kitakuwa jeneza
Na nyumba yako iyakuwa kaburi
Jamaa zako watakutupia udongo,nkwa heri ya milele!
Tu mavumbi sisi, tutarudi mavumbini *2n{ Roho ndiyo roho ndiyo itiayo uzima
Mwili haufai kitu } * 2
Tu mavumbi sisi, tutarudi mavumbini
Tazameni mimea, shambani
Matunda na maua, vyapendeza
Vyote vitanyauka
Wanyama wa pori, na nyumbani
Na ndege angani, wapendeza
Wote wataangamia
Ee ndugu sasa utubu rudi
Mrudie Mungu wako
Kwa maana duniani sisi ni wasafiri
Hujui saa na siku ndugu ya kuiacha dunia
Kwa maana duniani sisi ni wasafiri
Sayari angani zapendeza
Mito na mabonde duniani
Vyote vitatokomea
Mungu ndiye peke ajuaye
Siri ya maisha ya viumbe
Vyake ulimwenguni
{ Siku zinapita, miaka yapita
Neno lake Bwana halitapita kamwe }*2
Tu mavumbi sisi, tutarudi mavumbini * 2