Chorus
{Ee Bwana Mungu wangu
Tembea nami usiniache kwenye dunia (hiyo)
Ya machafuko } *2n
Nikianguka, Bwana, uniinue Bwana
Nikiteleza, Bwana, unishike mkono
Uniepushe na maadui wa roho yangu
Uniepushe na maadui wa roho yangu
Verse 2
Tazama ninaishi kwa mashaka na hofu kubwan(Kwani) Baadhi ya wanadamu wenzangu wamegeuka
Kuwa ni maadui zangu,
Wananiwinda wanikamate wavinyokoe viungo,
Eti wajipatie mali.
Verse 3
Tazama ninaishi kwa mashaka na hofu kubwan(Kwani) Baadhi ya waathirika wenzangu wamekamatwa
Bwana na wameshauawa,
Wamewakata vichwa na mikono, na miguu yao Bwana,
Eti wajipatie mali
Verse 4
Tazama sisi wanao wakiwa twakimbilia (kwako)n(Kwako) twazikabidhi roho zetu mikononi mwako
Maana ni wewe kimbilio
Usituachie adui zako watutie mikononi
Bwana utushike mkono