Tazama Wazazi

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Christmas,Advent,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Lent,Ordinary Time,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,Marian,Ordinary Time,MarianThanksgiving
Verse 1

Tazama wazazi wazuri nilio nao

Ni baba na mama walioyatenda haya

Nidhamu na sala wamenifundisha kwa bidii

Mapendo na wema wamenipa toka utotoni

Sasa nitaimba nimsifu Mungu kwa zawadi hii

Kwa zawadi hii ya wazazi alionipa

Chorus

Nikifikiria kiumbe wa Mungu mimi

Nikifikiria ukuu wa Mungu kwangu

Nikitafakari na matendo, anayotenda

Kwa maisha yangu na wazazi, na ndugu zangu

Ninashindwa kuyaelezea kwa kinywa changu

Nitakaa kwake niyatafakari haya

Verse 3

Tazama tazama elimu niliyo nayo

Kumbuka wengine hakujaliwa hiyo

Kwa nguvu ya neno na roho wake mtakatifu

Kanipa nafasi ili nitumike kwa wengine

Sasa nitaimba nimsifu Mungu kwa zawadi hii

Kwa zawadi hii ya elimu aliyonipa

Verse 4

Tazama tazama nchi hii nzuri nilimo

Wengine za kwao hazina amani kamwe

Amani furaha upendo na ukarimu huunuzuri wa watu wa mito milima na mabonde

Sasa nitaimba nimsifu Mungu kwa zawadi hii

Kwa zawadi hii ya nchi nilimozaliwa