Chorus
{ Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza
Ndugu wakae pamoja, pamoja kwa umoja
Ndugu wakae pamoja kwa umoja } *2
Verse 2
Ni kama mafuta mazuri mazuri kichwani
Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni
Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake
Verse 3
Kama umande wa Hermoni, ushukao milimani pa Sayuni
Maana ndiko Bwana alipoamuru baraka naam uzima hata milele