Verse 1
Tawi limechipuka shinani mwa Yesu
Kama tulivyopashwa habari na wazee
Likatoa ua, wakati wa usiku, lililochanua
Verse 2
Isaya alitaja ua hilo zuri
Ni Yesu mponya wetu, Maria alimzaa
Usiku mtulivu, uwezo wake Mungu, umefanya hivi
Verse 3
Na ua hili dogo lanuka vizuri
Lang'aa kama jua, giza lafukuza
Ni Mwana wa Mungu, hata mwana Adamu, Mwokozi wa watu
Verse 4
Siku ya kufa kwetu, Yesu tuongoze
Tuiache dunia, twende furahani
Mbinguni kwa Mungu, pale tutakusifu, milele daima