SectionsExitTanzania

Tanzania

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,MarianExit
Verse 1

Mwenyezi Mungu Rahimu na mradhi mwema,nsalamu salamu Mwumba wa Adamu

Watanzania tumekuja kwa wimbo,nna tenzi kuongea nawe leo hii

Uchaguzi mkuu huu tunaoandaa,ntwaomba ujae baraka zako kuu

Kusudi uwepo wako udhihirike,nkatika serikali tutakayounda

Verse 2

Rais mpya awe fimbo bora,nawe taa ya kweli kwenye kinara

Wabunge wawe matawi mazuri,nyenye kuzaa kwenye mti wa rutuba

Madiwani wawe watu wa watu,nkuongoza watu kwa ajili ya watu

Tujenge Tanzania madhubuti,nmioyoni badala ya ardhini

Verse 3

Wagonjwa wapone, makiwa wafarijiwe,nmasikini waonje maziwa kila siku

Wajane waishi, yatima waende shule,nfukara waone thamani ya utu wao

Majanga yakome, majeruhi watibiwe,nwalio gerezani wawe huru mitaani

Undugu ukue, amani iongezeke,nna wahalifu wote wabadilishe tabia

Verse 4

Na watoto, watoto wadogo,nwalelewe kwa maadili

Madhehebu, yote ya kidini,nyawe tahadhari ya upendo

Navyo vyama, vyetu vya siasa,nviwe siri kuu ya amani

Ibilisi, afunge virago,naondoke kamwe asirudi!n

Verse 5

Kiapo atakachoapa rais mpya,nkidumu hata hatimamu ya dahari

Majaribu yote yatakayotukumbuka,nyapimwe yasizidi kimo chetu

Mwenyezi Mungu rahimu twakuomba,ntulinde tulinde bila ya kuchoka

Ili mwisho wa safari ya hapa,ntufike mbinguni wote Tanzania