SectionsExitTalanta Tulizopewa

Talanta Tulizopewa

Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Chorus

{ Talanta tulizopewa na Mungu (Mwenyezi)

Tuzitumieni kwa kujipatia utakatifu } *2

Verse 2

Kama wewe ni baba wa familia

Au kama wewe ni mama wa familia

Kama wewe ni kasisi kanisani

Au kama wewe mtawa kanisani

Vyema utimize wajibu wako upate utakatifu *2

Verse 3

Kama wewe ni hakimu toa haki

Au kama wewe askari tenda haki

Usionee wanyonge masikini

Acha rushwa acha dhuluma tenda haki,

Vyema utimize wajibu wako upate utakatifu *2

Verse 4

Kama wewe dakitari au nesi

Hudumia wagonjwa wote kwa upendo

Mashambani maofisini wajibika

Acha uvivu fanya kazi kwa bidii,

Vyema utimize wajibu wako upate utakatifu*2

Verse 5

Viongozi na watawala tenda haki

Kumbukeni mtaulizwa na Muumba

Walimu nanyi fundisheni maadili

Nanyi wafanya biashara tenda haki

Tutaulizwa juu ya talanta alizotupa Muumba *2