Chorus
Sitawaacha nyinyi kama yatima,
Sitawaacha nyinyi (Acha nyinyi) asema
Bwana (ee Bwana) (Naja kwenu mioyonyenu ijae, furaha na amani,
Asema Bwana) *2 eeh
Verse 2
Nitawaombea nyinyi kwa Baba yangu
Naye atamtuma Roho wa kweli
Huyo Roho Baba atakayemtuma
Ndiye atakayewafariji mioyoni
Verse 3
Utukufu ulionipa ee Baba
Nimewapa na wao ili wapate
Kujua ndiwe peke uliyenituma
Ukawapenda wao ulivyonipenda
Verse 4
Baba hao ulionipa nataka
Wawe pamoja nami, nami popote
Popote kutazama utukufu wako
Utukufu ulionipa, anasema Bwana
Verse 5
Baba si hao tu ninawaombea
Lakini nao wale wataoniamini
Wote wawe umoja kama we Baba
Ulivyo ndani yangu nami ndani yako
Verse 6
Sitawaacha nyinyi kama yatima
Waipeleka roho, yako e Baba
Nawe unaufanya uso wa nchi
Uso wa nchi upya, anasema Bwana