SectionsExitSisi Wana Wa Dunia

Sisi Wana Wa Dunia

Ordinary Time,MarianExit
Chorus

Sisi wana dunia tukumbuke maneno,naliyosema Bikira Maria

Alipowatokea watoto wa Fatima,

Lucia Francis na Jacinta

Alisema tusali, tusali rosari, tupate amani

Na tuwaombee wale wakosefu wasio na mwombezi

Na wasiomwamini Yesu Mwokozi wamuamini ili waokoke

Verse 2

Mama yetu anahuzunishwa sana,nna matendo yetu maovu

Anajua adhabu yetu ijayo,nhivyo anaona huruma sana

Verse 3

Atusihi tuache dhambi kwa dhati,ntuache kumkosea Yesu

Tuyatubu makosa yetu yote,nili Bwana atupatie amanin

Verse 4

Tusitende maovu na dhambi,natusihi mama wa Yesu,

Tusimkasirishe tena Mungu,nasije tutupa motoni milele

Verse 5

Ibada ya moyo safi wa Maria,ntuizingatie daima,

Tupokee komunio takatifu,nkila Jumamosi ya kwanza ya mwezin