Chorus
{Siri ya moyo wangu, ni kilio changu
Na kilio cha moyo wangu, niione huruma yako } *2
Mungu wangu kinga yangu, nakuita Bwana
Ukinigeuka wewe nimekwisha mimi
Wewe ndiwe fimbo yangu, kimbilio langu
Ndiwe boma la wokovu, msaada wangu
Niepushie makucha ya dunia
Verse 2
Kikombe cha uchungu nimekunywa kwa harakwa
Sasa kimenikwama
Nimenaswa nimefikwa yamenikuta mimi
Ee Bwana ninakuita mimi ee Mungu njoo unikamilishe
Verse 3
Najua haina thamani, sala yangu ni chafu
Ibada haifai
Nimkimbilie nani zaidi yako wewe
Naililia huruma yako, mkono wako nishike Bwana
Verse 4
Mimi sistahili kabisa kupokea neema
Kutoka kwako Bwana
Ni mchafu ni mdhambi, nimeoza moyoni
Mikono nakuinulia Bwana, machozi yangu nafukia mimi