Siri Ya Mafanikio
Nikateleza nikatapatapa,nsauti ile ikanirudia tena
Ikanambia usiwe na hofu,ninua macho yako kwenye mti huu (na kisha)
Tazama tundu hili takatifu la neema
Kwenye moyo uliojaa pendo
Na ndilo siri ya mafanikio ya maisha
Ya furaha na amani ya kweli (aleluya)
Wa Yesu umefunuliwa moyo huo
Nauona uko wazi moyo ( tukufu)
Unanimiminia neema moyo huo
Uko wazi uko wazi moyo
Ulipochomwa kwa chuma kigumu,nna ni ugumu ule wa mioyo yetu
Ukatujibu kwa kumwaga maji,nmaji laini nayo damu ya sadaka (lakini)
Hauchukii hauna kisasi,nmoyo mpole mwema na mnyenyekevu
Shida na tabu tukiukabidhi,nunachotoa ni neema na ushindi
Mahangaiko na kumaka kwetu,ntuupelekee moyo wake Yesu
Tutafurahi tutafanikiwa,ndamu na maji yake yatatutakasa (lakini)
Ili daima atukuzwe Baba,nna mwana atukuzwe Roho Mtakatifu
Ilivyokuwa toka kule mwanzo,nsasa na siku zote daima milele (amina)