Chorus
Tumshangilie Mwokozi amefufuka
Tupige makofi, pia na vigelegele
Amefufuka Kristu mshindi na ukombozi umekamilika
Kwa ufufuko wake Kristu sisi tumekombolewa
Amefufuka mfalme mshindi, Simba wa Yuda anaonguruma
Na ikulu ya Ibilisi sasa imebomolewa
Verse 2
Amefufuka Mkombozi wetu Yesu Kristu
Kashinda dhambi na mauti ametukomboa
Utawala wa ibilisi umetoweka
Minyororo ya utumwa wa dhambi imeshavunjwa
Verse 3
Mayahudi waliomuua Bwana Yesu
Wameumbuka kwani mkombozi yuko hai
Na lile jiwe walilokataa waashi
Ndilo limekuwa jiwe kuu tena la pembeni
Verse 4
Nasi tukitaka kufufuka naye Kristu
Tuache dhambi za vilema vyetu kudumu
Kwani Yesu aliyefufuka ameleta
Uzima mpya kwa wale watakaobadilika