SectionsThanksgivingShukrani Yangu

Shukrani Yangu

Ordinary Time,MarianThanksgiving
Verse 1

Hii sio hadithi ninataka kusimulia

Wala sio historia wala si somo la siasa

Ni mambo mema sana aliyotenda Mungu kwangu

Na nisipoyatamka nitakuwa sina fadhila

Chorus

Wazazi wamenilea mpaka nimefika hapa

Majirani na ndugu zangu pia wamenipiga jekin[ b ] Baba usikie sala hii mimi natoann

Chorus

n{ Wabariki wazazi wangu wape maisha marefu

Wabariki na ndugu zangu wape amani tele

Marafiki zangu pia mimi mwenyewe

Siwezi kusahau kuwaombea na adui zangu } *2

Verse 4

Mungu ninakushukuru, afya njema wanijalia

Kila ninapoamka sijui nitakupa nini

Masomo yangu nasoma pia ninafaulu vyema

Sasa nimefika hapa sio kwamba mimi ni mwema

Verse 5

Shuleni niliposoma nilikuwa na marafiki

Waliosoma vizuri pia na wenye afya njema

Sio wote waliweza kufikia nilipofika

Nashindwa niseme nini jinsi umenipenda mimi

Verse 6

Vijijini nimeishi watu wengi nimewaona

Hawana mbele na nyuma wameishia kunywa pombe

Maisha yao magumu elimu yao haba haba

Nashindwa nikupe nini hapa nilipofika mimi

Verse 7

Siwezi kusema mengi najua wewe ndiwe kinga

Nibariki nijalie maisha yenye kupendeza

Kipaji nilicho nacho cha kuimba na kuhubiri

Kiwavute watu wengi wakuabudu wewe Bwana