SectionsExitShukrani Ya Mwili

Shukrani Ya Mwili

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Easter,Easter,Ordinary TimeExit
Verse 1

Nimeunakishi mwili wangu kwa marashi na kwa saluni

Na nimeulisha chakula safi na ukashiba

Nimehangaika kuupamba - kwa mavazi ya kupendeza

Na nikaunywesha kila kinywaji ukaburudika

Chorus

Tazama shukrani ya mwili huu ni uchovu na ugonjwa

Shukrani ya mwili kwangu ni usingizi

Shukrani ya mwili huu ni kutorithika kamwe

Shukrani ya mwili kwangu ni kurudi mavumbini, milele

Milele milele hazina yangu mbinguni (kweli) *4

Verse 3

Nimeuhifadhi kwenye nyumba ya kifahari na geti kubwa

Na nikaajiri mlinzi bora wa kulinda nchi

Nimeuhifadhi kwa mashuka chandarua na makapeti

Na nikaulaza kwenye gondoro yenye raha tupu

Verse 4

Nimeushibisha kwa anasa na starehe za kila namna

Na hata zile zinazotumia mwili wa wengine

Nimeukusanyia kiburi cha ujanja na ujuaji

Na nikaupatia utukufu machoni pa watu