SectionsExitShangilieni Harusi

Shangilieni Harusi

WeddingExit
Chorus

Yelele lele, yelele lele, leo tunayo furaha tele tele

Twasherehekea arusi ya wenzetu

Wamejitolea kwa moyo wao wote

Twasherehekea yote wametimiza

Arusi leo shangilia aa, shangilieni maarusi hawa

Arusi leo furahia aa, furahieni maarusi hawa

Verse 2

Twaombea baraka zake Bwana

Munapoanza maisha haya mapya

Shetani asiwatenganishe kamwe

Mubaki ndani ya Bwana Mungu wetun

Verse 3

Ewe mwanaume umpende mke wako

Kwani hiyo ndiyo amri ya Mungu wetu

Nawe mwanamke umpende mume wakao

Ndipo ndoa yenu isimame imara

Verse 4

Msiwasahau wazazi wenu pia

Kwani hao ndio nguzo ya masha yenu

Watoto wenu na muwatunze vema

Muwapeleke kwa kanisa ya Bwana

Verse 5

Na sisi sote tulioshuhudia

Arusi yenu siku hii ya leo

Twawahimiza mheshimu ndoa yenu

Kwani ndoa ni sakramenti takatifun

Verse 6

Yelele lele, yelele lele

Shangilieni maharusi hawa, furahieni maharusi hawa