SectionsEntranceSauti Za Kuimba

Sauti Za Kuimba

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary TimeEntrance
Chorus

Sauti za kuimba ni talanta zawadi (Tumepewa ) na Mungu tumwimbie } *2

Haya basi nyanyukeni tumsifun{Ninyi waimbaji (pazeni) zipaazeni sauti (hubirini) kwa sauti zenu } *2

Verse 2

Mwimbieni Bwana kwa ala za muziki zote zenye sauti tamu

Mpigieni ngoma na baragumu

Aee za muziki zote zenye sauti tamu

Mpigieni ngoma na baragumu

Verse 3

Jongeeni enyi watunzi wachezaji wa vinanda na waimbaji

Jiungeni nasi sifiche vipaji

Aee wachezaji wa vinanda na waimbaji

Jiungeni nasi sifiche vipaji

Verse 4

Sauti ya kwanza na pili wapendeza wanapoimba pamoja na

Na sauti ya tatu na nne ona

Aee wapendeza wanapoimba pamoja na

Na sauti ya tatu na nne ona

Verse 5

Kusifu kwapendeza sana duniani pia mbinguni ni furaha

Haya msifuni kuimba ni raha

Aee duniani pia mbinguni ni furaha

Haya msifuni kuimba ni raha

Verse 6

Kuimba huondoa dhiki ni faraja kwa waliokata tamaa

Ama burudani kwa walozubaa

Aee ni faraja kwa waliokata tamaa

Ama burudani kwa walozubaa

Verse 7

Sauti zenu ni talanta amueni jinsi mtazi-tumia

Angalieni mimi ninamwimbia

Aee amueni jinsi mtazi-tumia

Angalieni mimi ninamwimbia