SectionsEntranceSauti Inavuma

Sauti Inavuma

Ordinary Time,Ordinary Time,Ordinary Time,EasterEntrance
Chorus

Sauti inavuma (kulia), sauti inavuma (kushoto)

Sauti inavuma pande zote zinatikisika ulo

Dunia inanesa (kabisa), mbingu zinafurahi (lazima)

Watumwa wako huru, wanaimba na kumshukuru Mungu

Hii ni siku yetu, ya kubadilika na kutakata

Kuvua utu wa kale, na kuvaa, kuvaa utu mpya leo

Kwani mwalimu wetu, walimning`iniza na kumuua

Kaachana na kaburi ni mzima kama alivyokuwa mwanzo

Tunaimba aleluya, eeh eh aleluya,

Tunaimba aleluya, tunamshukuru aliye juu

Ngoma tunamchezea, tunamchezea,

Vigelegele vya nguvu vinaambatana na makofi

Tunapiga makofi makofi, makofi tu.

Verse 2

Ya kibinadamu kayaishi kama, kama vile tulivyo sisi (kabisa)

Na halafu akabadilika akavaa mwili wa utukufu

Verse 3

Lengo lake atuelimishe hivi, hivi kabisa tulivyo sisi (kabisa)

Tujitahidi kubadilika na kuvaa hali ya utukufu

Verse 4

Tukubali maumivu yote tena tujikane bila kusaza (fahali)

Makusudi tuzisalimishe hizi nafsi zetu kwa Mungu wetu