SectionsOffertorySasa Ni Wakati Mzuri

Sasa Ni Wakati Mzuri

Ordinary Time,Ordinary TimeOffertory
Chorus

Sasa ni wakati mzuri twendeni madhabahuni,

Tukatoe sadaka zetu, tulijenge kanisa la Mungun{ Ewe ndugu yangu mkristu,

Changamka, changamka, peleka sadaka kwa Bwana.

Nenda katoe kwa moyo mweupe

Uzipate baraka za Mungu } *2

Verse 2

Mkristu kutoa sadaka,

Ndio wajibu wa kila mmoja,

Hivyo mkristu kumbuka wajibu,

Nenda katoe sadaka kwa Bwana.

Verse 3

Mwambie Bwana Mungu wako,

Baba pokea nilichokileta,

Hiki ndicho ulichonijalia,

Nakutolea kama shukrani.

Verse 4

Zamani za mababu zetu,

Walipeleka sadaka za nyama,

Nasi wakristu wa leo twendeni,

Tupeleke fedha za mifukoni.