Chorus
Salamu salamu Malkia wa Mbingu
Salamu salamu, Mama wake Mungu
Sisi wana wako, twaja mbele yako
Tupokee mama sisi wana wako
Verse 2
Kukupenda wewe ndiyo heri yetu
Kukuomba wewe tumaini letu
Ewe mama mpole, mwenye uso mpole
Utuhurumie utusaidie
Verse 3
Yesu kakupenda akakuchagua
Kuwa mama yake akakuteua
Umebarikiwa, umejaa neema
Jina lako Baba litukuzwe pote
Verse 4
Hapa duniani utusaidie
Na adui mwovu utuepushie
Utuangalie utusaidie
Ee mama mwezaji utusaidie