SectionsExitSalamu Salamu Malkia Wa Mbingu

Salamu Salamu Malkia Wa Mbingu

Ordinary Time,MarianExit
Chorus

Salamu salamu Malkia wa Mbingu

Salamu salamu, Mama wake Mungu

Sisi wana wako, twaja mbele yako

Tupokee mama sisi wana wako

Verse 2

Kukupenda wewe ndiyo heri yetu

Kukuomba wewe tumaini letu

Ewe mama mpole, mwenye uso mpole

Utuhurumie utusaidie

Verse 3

Yesu kakupenda akakuchagua

Kuwa mama yake akakuteua

Umebarikiwa, umejaa neema

Jina lako Baba litukuzwe pote

Verse 4

Hapa duniani utusaidie

Na adui mwovu utuepushie

Utuangalie utusaidie

Ee mama mwezaji utusaidie