Chorus
Sala yangu ipae mbele yako Bwana * 2n{ Kama moshi wa ubani altareni,
Na kuinuliwa kwa mikono yangu
Iwe kama sadaka, sadaka ya jioni } * 2
Verse 2
Ee Bwana tunakutolea sadaka yetu,
Pamoja na maisha ya kila siku.
Verse 3
Uwe radhi kuipokea sadaka yetu,
Kama zile za mababu wa zamani.
Verse 4
Hivyo sadaka ifane mbele zako Bwana,
Na iwe sadaka ya shukrani kubwa.
Verse 5
Nasi utubariki maisha yetu yote,
Na mwisho utujalie heri yako.