SectionsExitSafari Ya Mafinikio

Safari Ya Mafinikio

Ordinary Time,MarianExit
Chorus

Safari ya mafanikio ni ngumu sana

Ukiwa na imani haba itakushinda

Unapoianza safari bahari imetulia

Unapata matumaini ya kumaliza salama

Ukifika katikati mambo hubadilika

Ni mawimbi na vikwazo misukosuko mingi

Usikate tamaa, jipe moyo utashinda * 2

Verse 2

Utapata machukizo na matatizo mengi

Ndiyo hali ya dunia, yote uvumilie

Utapata mitihani, migumu ya maisha

Ndiyo hali ya dunia, yote uvumilie

Verse 3

Utapata vishawishi vingi vya ulimwengu

Ndiyo hali ya dunia vyote uvumilie

Utapata marafiki wema nao wabaya

Ndiyo hali ya dunia wote wavumilie

Verse 4

Utapata masumbuko na maradhi ya ajabu

Ndiyo hali ya dunia yote uvumilie

Kaza mwendo ndugu yangunkaza mwendo kwenye nuru

Songa mbele e Mkristu yote uvumilie