SectionsExitSafari Ni Moja

Safari Ni Moja

Ordinary Time,MarianExit
Verse 1

Twajua Mbingu iko mbali na njia ndefu,ntena mitego ni mingi kila kona,nlakini tumaini liko karibu nasi,nkwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu,

Naye atatuongoza tukimwamini,nmpaka tufike salama tuendakoo.

Chorus

Safari ni moja tena na njia ni moja (aa)

Hatua ni moja moja foleni ni moja(naa)

Mlango mmoja tena mlango mwembamba,n(twendee) twende tuingie tukaishi huko milele *2

Verse 3

Shetani hakuanza leo kutuvuruga,ntangu pale kwenye mti bustanini,nkavunja ujamaa mwema wa Babu zetu,nwakamkosea Mungu Wakaanguka,nnao wakajihukumu wakajificha,nwakitaka wapotee mbali naye.

Verse 4

Ya Mbingu yakajinyenyekeza duniani,

Laana ikatakaswa kwa sadaka,nya mti yakavunjwa vunjwa juu ya mti,nya bustanini yakashindwa mlimani,naibu ya Mwanadamu ikaondoka,nakaandaliwa Ufalme Mbinguni.

Verse 5

T/B: Tutazame mbele na tusigeuke nyuma,

Mwokozi wetu Yesu Anatungojea.n

Chorus

Wote: Safari ni moja safari moja,

Twendeeni pamoja safari moja,

Ipande milimani ni moja safari moja,

Ishuke Mabondeni ni moja safari moja,

Inyeshe liwake ni moja safari ni moja tuu.