Chorus
Sadaka yetu Bwana, twaomba upokee
Ni mazao ya mashamba yetu ee Baba upokee *2
Verse 2
Mkate na divai, na pia nafsi zetu
Ni zawadi yetu kwako, ee Baba upokee
Verse 3
Na fedha za mifukoni,mazao ya mashamba,
Ee Baba, kazi zetu, twaomba upokee(sadaka)
Verse 4
Pokea na nyoyo zetu, miili yetu pia
Ee Baba utupokee, tulio wana wako(sadaka)
Verse 5
Pokea tunakuomba, ingawa ni kidogo
Kwa unyenyekevu Baba, tunavileta kwako
Verse 6
Zawadi hii twaitoa, kwa sifa yako wewe,
Kwa ajili yetu sisi, nazo jamaa wetu (sadaka)