Chorus
{ Sadaka ya uchungu na kitubio cha machozi
Vitanifaa nini kama nisipolainisha moyo } *2
Verse 2
Moyo wangu mgumu tena mgumu kama jiwe
Na kumwagia maji juu ya jiwe kazi bure
Verse 3
Nisipolitangaza pendo la Mungu kwa vitendo
Kamwe sitazionja baraka na rehema zake
Verse 4
Na nisipoikiri kanuni ile ya imani
Hata nikeshe mimi kwa maombi ni kazi bure
Verse 5
Ni heri nikubali kikao cha upatanishi
Nimkane shetani na nguzo zake nizivunje