SectionsOffertorySadaka Ya Kuazima

Sadaka Ya Kuazima

Ordinary TimeOffertory
Chorus

Jiandae wiki nzima weka tayarinsadaka yako mkristu (toa kwa moyo safi)

Usitoe kwa uchoyo wala sadaka ya kuaziman{(jasho lako) umtolee Mungu alicho kupa hahitaji zaidin(maana) Vitu vyote mali yake toa kwa ukarimu } *2

Verse 2

Ninaona hasara kutoa (nanung'unika)

Bwana ona mi nilivyo changanyikiwa

Mara nyingi naomba jirani (hapa kitini)nsiyo yangu ni sadaka ya kuazima

Verse 3

Ninaona uchoyo kutoa (sadaka yangu)nninaleta kidogo tena kwa uchungu

Mara nyingine sitoi kitu (nilicho nacho)nninaficha sadaka yangu mfukoni

Verse 4

Ninaona aibu kubaki (ni wasiwasi)nnimeketi nao wengine wanatoa

Mara nyingine hata siendi (nimekimbia)nkanisani ninahepa michango nyingi

Verse 5

Wana baraka wanaotoa (kwa moyo ule )nwa Abeli wa Ibrahimu na Isaka

Bwana Mungu haipendi sadaka (yake Kaini)nwala yule Anania na Safira