Verse 1
Bwana roho zetu zatamani - hayo maji yenye uzima
Bwana roho zetu zina kiu tupe maji hayo ya uzima
Ee Bwana tuna kiu tunyweshe
Tuna kiu ee Bwana tupe maji hayo ya uzima *2
Verse 2
Wewe ndiwe taa ya maisha wewe ndiwe mweza wetu
Wewe ndiwe mwanga wetu sote utatuongoza daima
Ee Bwana tunkuja daima tuko nawe
Ee Bwana utatuongoza daima
Verse 3
Wewe ndiwe nguvu yetu sote wewe ndiwe mweza vyote
Tupigwapo kumbo na shetani wewe ndiwe tulizo letu
Ee Bwana tuongoze daima maishani
Ee Bwana tupe nuru yako njiani *2