Posho Langu

Marian,Ordinary TimeEucharist
Chorus

Bwana ndiye fungu la posho langu,

Na la kikombe changun{Wewe unaishika kula yangu,

Nimemwambia Bwana, Bwana

Wewe ndiwe Bwana wangu } *2

Verse 2

Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri

Na mtima wangu, umenifundisha usiku

Nimemweka Bwana mbele yangu daima

Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu sitaondoshwa

Verse 3

Kwa hivyo moyo wangu, unafurahi moyo wangu

Washangilia, nao mwili wangu utakaa

Kwa kutumaini, Maana wewe Bwana

Hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu

Verse 4

Utanijulisha njia, njia ya uzima

Mbele ya uso wako, ziko furaha tele,

Na katika mkono wako wa kuume

Mkono wa kuume mna neema ya milele

Verse 5

Mungu nihifadhi mimi, maana nakukimbilia

Wewe Mungu wangu, Bwana ndiwe Bwana wangu,

Wewe Bwana ndiwe fungu la posho langu

Na la kikombe changu wewe unaishika kula yangu