SectionsThanksgivingPokea Hii Pete

Pokea Hii Pete

Lent,Wedding,Ordinary Time,WeddingThanksgiving
Verse 1

Pokea hii pete ee mwenzangu,

Iwe ishara ya pendo langu, na uaminifu wangu kwako

Chorus

{ Nakupenda hakika, nakupenda ajabu

Wewe wangu daima mimi wako wewe

Tutaishi pamoja, tutakula pamoja

Hadi kifo kifike, kitutenganishe } *2

Verse 3

Jukumu langu ni kukupenda,

Wakati wa raha na wa shida, na wewe kwangu weka heshima

Verse 4

Safari hii ndefu ya maisha,

Imeanza leo siogope, tutatembea bila kuchoka

Verse 5

Milima mabonde ya maisha,

Tutapanda tena tutashuka, tukiwa pamoja siku zote