SectionsExitPilka Pilka

Pilka Pilka

Lent,Wedding,Ordinary TimeExit
Verse 1

Pilka pilka kila siku watu wa dunia

Wanahangaika kutafuta mali za dunia

Asubuhi ni msongamano, mchana vilevile

Usiku shughuli zafanyika kama kawaida

Chorus

Tafuteni kwanza ufalme ule wa mbinguni

Na hayo mengine (hakika) mtazidishiwan{Yeye Mungu (Mwenyezi) mtetezi (ajabu)

Mkiamini atawashughilikia } * 2

Verse 3

Pilika pilika watu wengi kutafuta elimu

Hawakumbuki kwamba Yesu ni mwalimu tosha

Ajali nyingi barabarani zinafanyika kwetu

Tumesahau kwamba Yesu ni dereva tosha

Verse 4

Pilika pilika twatafuta hospitali kubwa

Huku daktari mkuu ni Mungu wa majeshi

Watu watafuta waganga ili wapate mali

Bali Mungu wa mbinguni ndiye mmliki wa vyote

Verse 5

Pilika pilika tunawaza usiku na mchana

Vile tutakula vizuri na kuvaa vizuri

Kwani ndege wale wa angani wanalishwa na nani

Kama siyo Mungu wa mbinguni basi huyo nani

Verse 6

Pilika pilika wenzangu tumuelekee Mungu

Tusifadhaike bali tuwe na matumaini

Atatujalia mema mengi tukiwa duniani

Mwisho tutafurahi na Yesu kule juu mbinguni