SectionsExitPendo La Marafiki

Pendo La Marafiki

Ordinary Time,Ordinary Time,Christmas,Ordinary Time,Ordinary TimeExit
Verse 1

Ninyi ndinyi mmenikamilisha kamilisha (hadi)

Hadi nikawa hi-vi mi-mi nilivyo (ndugu zangu)

Ni Mungu Baba ndiye aliyetukutanisha (japo)

Japo hatulingani tumekamilishanan{Katika pendo lenu - ndipo nimeelewa jinsi Mungu alivyo

Nimemuona - Mungu macho kwa macho } *2

Chorus

[ s ] Nikiwa na njaa -

Ni ninyi marafiki zangu mnimegeao mkaten[ a ] Penye machungu na maumivu makali -

Ni ninyi marafiki zangu mwaniuguza majerahan[ t ] Nikitawaliwa na hofu -

Ni ninyi marafiki zangu mnaonipa moyo upyan[ b ] Tena nikipotea njia -

Ni ninyi marafiki zangu mwanirudi mwanikosoan

Verse 3

Ona tunavyosaidiana hima, wenyewe kwa wenyewe,

Wakati wa furaha hata wa shida

Tumeweka mbali tofauti kidaraja na mali

Bahati iliyoje kuwa pamoja

Verse 4

Ona chuki, wivu, fitina, umimi, havimo kati yetu

Wakati wa furaha hata wa shida

Tumeweka msingi imara usiotikisika

Bahati iliyoje kuwa pamoja

Verse 5

{ Pendo pendo pendo pendo -npendo letu lidumu milele

Tuombeane tusaidianeni -nwaone Mungu kati yetu } *2

Wasitenganishwe - wapendanao

Waombeeni - baraka telensitenganishwe - wapendanao

Waombeeni - baraka tele, pendo na lidumu