SectionsEntrancePasipo Makosa

Pasipo Makosa

LentEntrance
Verse 1

Pasipo makosa Mkombozi wetu,

Katika baraza la wakosefu

Na wote walia asulibiwe,

Aachwe Baraba na Yesu afe

Aachwe Baraba na Yesu afe

Verse 2

Ee Yesu washika msalaba wako,

Na unakubali kufa juu yake

Ee Yesu useme sababu gani,

Ya nini mateso makali hayo?

Ya nini mateso makali hayo?

Verse 3

Ni pendo kwa Baba wa uwinguni,

Ni huruma yangu kwa wakosefu.

Ewe mkristu kumbuka mateso yangu,

Uache makosa, uache dhambi

Uache makosa, uache dhambi