Chorus
Pangoni Bethlehemu, kazaliwa Mwana wa Mungu *2
Tuimbe wote aleluya, aleluya, aleluya,
Aleluya, ni furaha Bwana kazaliwa
Verse 2
Kazaliwa mtoto Masiha wetu, twende Bethlehemu tukamwabudu
Verse 3
Kazaliwa mtoto ndiye mfalme wetu, aja na ufalme begani mwake
Verse 4
Tulimsubiri sana huyo mfalme wetu, sasa ameshuka kutukomboa
Verse 5
Malaika Mbinguni wanamsifu Bwana, nao wanaimba nyimbo zashangwe
Verse 6
Nasi pia twendeni huko Bethlehemu, twende na zawadi tukamtolee